Wanawake wanaouza miili yao migodini Tanzania

Miaka ya hivi karibuni wanawake wamekuwa wakijitosa kufanya kazi mbalimbali za kiuchumi, miongoni mwa maeneo wanayofanyia kazi ni migodini.

Lakini wapo pia wanawake wanaofanya biashara isiyo halali katika sheria za Tanzania, biashara ya kuuza miili yao katika maeneo hayo hayo ya migodini.

Munira Hussein alitembelea mgodi wa North Mara uliyoko Kaskazini mwa Tanzania na kuandaa taarifa ifuatayo.