Kijana mvumbuzi wa mitambo Kenya

Kijana mvumbuzi wa mitambo Kenya

Katika eneo la Ongata Rongai, viungani mwa jiji la Nairobi, ukiingia katika chumba cha Peter Maina, unaweza kudhani umeingia katika karakana katika chuo kikuu au chuo cha kiufundi.

Kuna vifaa na mitambo ambayo hujawahi kuiona kwingine - utaona kigari ambacho kinadhibitiwa kwa kompyuta, kicheza muziki kinachojitanua, helikopta mfano ambayo inaweza kupaa, na pia kiti cha magurudumu ambacho kinaweza kupanda ngazi.