Rais Zuma ashutumu ghasia dhidi ya wageni A. Kusini

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amelaani kuzuka upya kwa tabia ya kuwashambulia wageni walioko nchini Afrika kusini.
Bwana Zuma amesema kuwa raia wengi wa kigeni wanaoishi Afrika Kusini, ni watu wanaoheshimu sheria na kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa hilo.
Amesema ni makosa kwa raia wa nchi hiyo kuwaona wageni kama ni walanguzi na watumiaji wa mihadarati.
Chanzo cha picha, Reuters
Raia wa Afrika kusini wakimshambulia raia wa kigeni wakati wa ghasia dhidi ya wageni nchini humo
Licha ya kauli hiyo ya rais Zuma waandamanaji tayari wamefunga barabara mjini Pretoria kwa kuchoma tairi za magari wakijiandaa kwa maandamano ya kupinga kile wanachotaja hali ya wenyeji kupoteza nafasi za kazi kwa wageni.