Wageni wajihami Afrika Kusini kujilinda

Makundi ya wahamiaji waliiojihami nchini Afrika Kusini

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Makundi ya wahamiaji waliiojihami nchini Afrika Kusini

Raia wa Kisomali wamejihami dhidi ya uvamizi wowote wa Wageni mjini Pretoria katika eneo la Marastabad nchini Afrika Kusini.

Kundi hilo lilikuwa linakabiliana na kundi jingine la raia wa Afrika kusini wanaoongoza ghasia dhidi ya wahamiaji.

Hatahivyo maafisa wa polisi waliingilia kati na kuwatimua kwa kutumia ndege aina ya helikopta pamoja na risasi za mipira.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Makundi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini

Takriban watu wawili wamejeruhiwa na risasi hizo za mipira wakati polisi walipokuwa wakitawanya maandamano dhidi ya wageni nchini humo.

Mpiga picha mmoja alipigwa risasi mbili za mipira mgongoni alipokuwa akirudi nyumbani kutoka shule.

Maafisa wa polisi wametumia ndege aina ya helikopta ,risasi za mipira na vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao kuzuia makundi ya wahamiaji yaliojitokeza yaliojihami na fimbo,mawe na visu.

Wanaharakti wa shirika la Save South Afrika wanasema kuwa Meya wa Johannesburg Herman Mashaba ana maswali mengi ya kujibu.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Maafisa wa polisi wawatawanya waandamanaji Afrika Kusini

Licha ya Bwana Mashaba kusema kuwa ghasia hizo hazina nafasi katika taifa hil,o wanaharakati wa shirika hilo wanadai kuwa matamshi yake kwamba wahamiaji nchini humo ndio wanaohusishwa na uhalifu ndio yaliosababisha ghasia hizo.