China: Marekani itatue mgogoro wake na Korea Kaskazini

Donald Trump kulia na Kim Jong un wa Korea kaskazini
Maelezo ya picha,

Donald Trump kulia na Kim Jong un wa Korea kaskazini

Serikali ya China imeitaka Marekani kuimarisha juhudi zake katika kuangazia mgogoro wake na Korea Kaskazini.

Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini China Geng Shuang amesema kuwa Washington na Pyongyang zinafaa kuchukua majukumu zaidi katika kuangazia hali ya wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini huku China ikiunga mkono juhudi hizo.

China hivi majuzi ilipiga marufuku uagizaji wa makaa kutoka Korea Kaskazini hatua inayoonekana kuathiri uchumi unaoyumba yumba wa taifa la Korea Kaskazini.

Hatahivyo rais wa Marekani Donald Trump wiki iliopita alisema kuwa China inawezakufanya mengi ili kutatua swala hilo ikitaka.