Mashirika ya habari yashtumu marufuku ya ikulu ya Whitehouse

Baadhi ya mashirika ya habari yameapa kutohudhuria mikutano yoyote ya habari ikulu iwapo marfuku hiyo itaendelea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Baadhi ya mashirika ya habari yameapa kutohudhuria mikutano yoyote ya habari ikulu iwapo marfuku hiyo itaendelea

Mashirika kadhaa makubwa ya habari yameelezea masikitiko yao kuhusu kitendo cha kukatazwa kuhudhuria mkutano wa waandishi habari huko ikulu ya White House.

Wasimamizi wa Gazeti The New York Times na shirika la utangazaji CNN wamesema hali hiyo haikubaliki kamwe na kuitaja kuwa ukiukaji wa katiba ya nchi hiyo.

Mkurugenzi wa shirika la habari wa the New York Times Dean Baquet amesema jambo kama hilo halijawahi kutokea katika historia ya gazeti hilo.

Amesema uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa kuweka uwazi kwenye shughuli za kiserikali kwa niaba ya maslahi ya umma.

Msemaji wa rais wa Marekani Donald Trump , Sean Spicer awali alikuwa amedai kuchukua hatua hiyo kwa sababu hawawezi kukaa kando na kuachia uenezaji wa habari za uongo.

Rais Trump amekuwa akiviita maadui wa raia wa Marekani vyombo kadhaa vya habari nchini humo ikiwemo CNN na The New York Times