Mwana wa Pele arudishwa gerezani Brazil

Edinho ni mwana wa gwiji wa soka nchini Brazil Pele
Maelezo ya picha,

Edinho ni mwana wa gwiji wa soka nchini Brazil Pele

Mwana wa gwiji wa soka wa Brazil Pele, amejisalimisha kwa maafisa wa magereza kwenda kutumikia kifungo alichohukumiwa kuhusiana na makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Edinho, ambae alikuwa mlinda lango wa timu ya klabu ya Santos nchini humo alikuwa ameachiwa huru wakati rufaa dhidi ya kifungo cha miaka 33 ilipokuwa ikisikizwa.

Lakini japo mahakama ya mjini Sao Paulo imeamua kupunguza kifungo hicho hadi miaka 12 imemtaka arudi gerezani wakati kesi ya rufaa aliyoiwasilisha ikiendelea kusikizwa.

Edinho kwa upande wake amekuwa akikana mashtaka hayo ya ulanguzi wa dawa za kulenywa.