Wema Sepetu akihama CCM na kujiunga na Chadema

Aliyekuwa malkia wa urembo nchini Tanzania 2006 Wema Sepetu
Maelezo ya picha,

Aliyekuwa malkia wa urembo nchini Tanzania 2006 Wema Sepetu

Aliyekuwa malkia wa urembo nchini Tanzania 2006 Wema Sepetu amekihama chama cha CCM na kujiunga na kile cha Chadema.

Amewaambia wanahabari nyumbani kwake huko Sinza kwamba amechukua hatua hiyo ili kupigania demokrasia nchini humo.

Baadhi ya wanachama wa Chadema na wafuasi pia walihudhuria hafla hiyo.

Alielezea mkasa alioupata akiwa mshukiwa wa kampeni ilioanzishwa na Kamishna wa eneo la Dar es Salaam Paul Makonda katika kipindi cha wiki mbili zilizopita kuwa ya kufedheheshwa na chama tawala.

''Wakati nilipokuwa nikizuiliwa niliteswa huku marafiki zangiu wakitishiwa na kuzuiwa kunitembelea kutokana na madai'',alisema.

Alisema kwamba alikifanyia mengi chama cha CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2015 kabla ya kufedheheshwa.

''Nimejiunga na Chadema sio kwasababu nina uchungu.

Ninataka kupigania demokrasia na heshima ya Watanzania.Ninaamini kwamba wafuasi wangu watajiunga na Chadema''.

Mamake Mariam Sepetu ambaye alikihama CCM na kujiunga na Chadema alisema kwamba ana uchungu na vile mwanawe alivyofanyiwa .

''Hiyo ni sababu tosha ya mimi kukihama chama cha CCM'',alisema.

Bi Sepetu alikuwa mwenyekiti wa CCM tawil la Nzasa.