Kim Jong-nam alifariki kati ya dakika 15 na 20

Wataalamu wakifanya uchunguzi uwanja wa Kuala Lumpur
Maelezo ya picha,

Wataalamu wakifanya uchunguzi uwanja wa Kuala Lumpur

Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alipewa kiwango kikali cha kemikali aina ya VX na aliaga dunia kati ya dakika 15 na 20, kwa mujibu wa waziri wa afya nchini Malaysia.

"Hakuna dawa ingefaulu kumuokoa," Subramaniam Sathasivam alisema.

Kim aliaga dunia wiki mbili zilizopita baada ya wanawake wawili kumkabili kwenye uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpur.

Maafisa wa usalama wa Malaysia wametangaza kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur ni salama baada ya kuuawa kwa Kim.

Awali, polisi walipekua jengo husika wakichunguza iwapo kulikuwa na sumu kali iliyotumiwa katika mauaji hayo aina ya VX, au sumu nyingine yo yote.

Maelezo ya picha,

Maelfu ya abiria wamepitia uwanja huo tangu kisa hicho kitokee

Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90, kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.

Wanabalozi wa Indonesia waliokutana na Siti Aisyah, wanasema aliwaambia kuwa wanaume wawili, walionekana kama Wakorea au Wajapani, walimpa mafuta yaliyofanana na yale ya mtoto kumpaka usoni mwanamme mmoja.

Mafuta hayo sasa yanafikiriwa yalikuwa na kemikali VX, moja kati ya sumu kali kabisa. Hadi sasa watu watatu wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo.

Maelezo ya picha,

North Korea has not identified the man who died as Kim Jong-nam, only as a North Korean citizen

Maelezo ya picha,

Siti Aisyah anasema alilipwa dola 90