Huenda kocha wa Mo Farah alikiuka sheria za dawa za kuongeza nguvu za mwili

Salazar (katikati) akishangilia na Mo Farah na Galen Rupp baada ya wawili hao kushinda dhahabu na fedha katika mashindano ya olimpiki ya London mwaka 2012
Maelezo ya picha,

Salazar (katikati) akishangilia na Mo Farah na Galen Rupp baada ya wawili hao kushinda dhahabu na fedha katika mashindano ya olimpiki ya London mwaka 2012

Ripoti iliyofuja inaonyesha kuwa Alberto Salazar, ambaye ni Kocha wa bingwa wa olimpiki Mo Farah, huenda alivunja sheria za dawa za kuongeza nguvu za mwili ili kuboresha matokeo ya wanariadha.

Ripoti hiyo ya kuanzia mwezi Machi mwaka uliopita ya shirika na Marekani la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za mwili Usada, ilipewa gazeti la Sunday Times na wadukuzi wa Urusi.

Inadai kuwa bwana Salazar huenda aliwapa baadhi ya wanariadha hao dawa ya kuongeza nguvu za mwili ya L Carnitine, ambayo inaruhusiwa kutumika kw kiwango kidogo.

Bwana Salazar na Mo Farad wote wamekana kukiuka sheria za kuzuia matumizi ya dawa hizo.

Shirika Usada linasema kuwa linaifahamu ripoti hiyo na linachunguza ikiwa sheria ilikiukwa.

Maelezo ya picha,

Salazar amekuwa akichunguzwa na Usada tangu mwaka 2015