Kiongozi wa Taliban awataka watu kupanda miti Afghanistan

Wapiganaji wa Taliban Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa Taliban

Kiongozi wa Taliban nchini Afghanistan Hibatullah Akhundzada amewashauri watu nchini humo kupanda miti zaidi.

Katika taarifa alitoa wito kwa raia na wapiganaji kupanda mti mmoja au zaidi kwa minajii ya kurembesha nchi.

Afghanistan inakumbwa na tatizo la ukataji miti, huku miti ikikatwa kwa kuni na biashara haramu ya mbao.

Si kawaida kwa Taliban kutoa taarifa zinazohusu mazingira.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu wengi nchini Afghanistan hutumia kuni

Akhundzada, ambaye alitangazwa kiongzi mwezi Mei mwaka uliopita, anafahamika kama kiongozi wa kidini kuliko kiongozi wa kivita.

Taliban ushiriki zaidi na uzalishaji wa bangi ulioharamishwa nchini Afghanistan na hutosa ushuru maeneo ambayo wanadhibiti.

Kundi hilo lilitawala sehemu kubwa ya Afghanistan kuanzia mwaka 1996 hadi wakatai lilipinduliwa muungano ulioongozwa na Mareknai mwaka 2001.

Haki miliki ya picha Afghan Islamic Press
Image caption Hibatullah Akhundzada ni msomi wa kidini kutoka Kandahar