Ufaransa kutuma wanajeshi Niger

Mwanajeshi wa Ufaransa
Maelezo ya picha,

Mwanajeshi wa Ufaransa

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa anasema nchi yake itatuma wanajeshi wa kupambana na ugaidi kwenda kusaidia jeshi la Niger, baada ya wapiganaji kuvizia na kushambulia wanajeshi waliokuwa zamu, na kuwauwa 15.

Jean-Yves Le Drian anasema kuwa wanajeshi wa Ufaransa wanapelekwa kufuatia ombi la kiongozi wa nIger, Rais Mahamadou Issoufou, baada ya shambulio la Jumatano karibu na mpaka wa Mali.

Inafikiriwa wanajeshi kama 50 hadi 80 watapelekwa Niger, na kuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilioko huko, kinacholenga wapiganaji wa Kiislamu katika eneo la Sahel.