Mashambulizi 10 hutokea kila siku dhidi ya wahamiaji Ujerumani

Mashambulizi dhidi ya sehemu wanamoishi wahamiaji ni mengi Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mashambulizi dhidi ya sehemu wanamoishi wahamiaji ni mengi

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa yametokea mashambulio zaidi ya 2500 dhidi ya wakimbizi nchini Ujerumani mwaka jana.

Watu zaidi ya 50 walijeruhiwa, wakiwemo watoto 43.

Mwaka 2016, ndio ulikuwa wa kwanza ambapo takwimu kama hizo zilianza kukusanywa.

Takwimu za wizara ya mambo ya ndani ya nchi, pia zinaonyesha kuwa vituo vya wakimbizi vilishambuliwa karibu mara elfu moja , sawa na mwaka uliotangulia.

Mwaka 2015, Ujerumani ilipokea wahamiaji karibu laki tisa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Idadi ya wanaoomba hifadhi Ujerumnai ilipanda mwaka 2016