Papa Francis kwenda Sudan Kusini

Italy Haki miliki ya picha AP
Image caption Papa Francis

Papa Francis amesema kuwa anatarajia kufanya ziara Sudani ya Kusini pamoja na askofu mkuu wa Canterbury, Justin Welby.

Papa ameeleza kuwa ziara yake itakua ya siku moja tu kutokana na kuwepo kwa usalama mdogo.

Papa aliongeza kuwa maaskofu wa sudan Kusini wamekua wakimtaka afanye ziara nchini humo ili ashuhudie athari ya njaa na vita kwa watu wa sudani kusini.

Aliyasema hayo alipotembelea kanisa la waanglikana jijini Rome Italia.