Mteule mwengine wa Trump akataa kuchukua wadhfa

Mteule mwemngine wa rais Donald Trump katika waziri wa wanamaji akataa wadhfa huo Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Mteule mwemngine wa rais Donald Trump katika waziri wa wanamaji akataa wadhfa huo

Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa maslahi.

Philip Bilden ameeleza wasiwasi wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika kujitenganisha na biashara zake.

Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo.

Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii