Baba ya mwanajeshi aliyeuawa akataa kukutana na Trump

Komando William Ryan Owen wa jeshi la wanamaji la Marekani Haki miliki ya picha CAPT JASON SALATA
Image caption Komando William Ryan Owen wa jeshi la wanamaji la Marekani

Babake mwanamaji wa Marekani aliyeuawa katika uvamizi wa wapiganaji wa al Qaeda mjini Yemen mwezi uliopita amesema kuwa alikataa kukutana na rais wa Marekani Donald Trump wakati mwili wa mwanaye ulipowasili Marekani.

''Sitaki kumuona alimwambia kiongozi mmoja wa dini wakati huo''.

Shambulio hilo la tarehe 28 mwezi Januari lilikuwa la kwanza lililoagizwa na Bwana Trump.

Bill Owens ambaye mwanawe William Ryan Owen aliuawa, aliambia jarida la Miami Herald kwamba serikali inafaa kumfanyia uchunguzi mwanawe.

Trump kuwazuia wahamiaji kuingia Marekani

Pena Nieto amjibu Trump

''Kwa nini kuwepo kwa ujumbe kama huo wiki moja baada ya yeye kuchukua mamlaka. Kwa nini''? Alisema katika mahojiano na gazeti hilo.

''Kwa kipindi cha miaka miwili hakuna mwanajeshi aliyeruhusiwa kuelekea Yemen, walikuwa wakitumia makombora na ndege zisizokuwa na rubani kutekeleza mashambulio kwa sababu hakukuwa na raia yeyote wa Marekani aliyekuwa akilengwa. Sasa mara moja tunachukua hatua hii''.

Uvamizi huo ulioagizwa na rais Trump siku sita baada ya kuchukua mamlaka unaaminika kuwaua raia kadhaa ikiwemo watoto.

Wamarekani 3 walijeruhiwa katika uvamizi huo uliodaiwa kuanza kupangwa na utawala wa rais Obama.