Oscars: Filamu yapewa ushindi kimakosa

Waigizaji wa filamu ya Moonlight wafurahia baada ya kubaini kwamba walishinda uzo la filamu bora

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Waigizaji wa filamu ya Moonlight wafurahia baada ya kubaini kwamba walishinda uzo la filamu bora

Hafla ya tuzo za Oscars imemalizika kwa kishindo cha mkanganyiko.

Filamu, Moonlight, inayosimulia hadithi ya mvulana mweusi anayeegemea mapenzi ya jinsia moja imechukua tuzo kuu ya filamu bora.

Awali filamu ya kimuziki LALA Land ilitangazwa kuwa filamu bora, na baada ya waigizaji wa filamu hiyo kuingia jukwaani tayari kutoa hotubao zao za ushindi, mmoja wa watayarishi wa Oscars akainglia na kutangaza kwamba Moonlight ndio mshindi halisi.

Kundi la waigizaji wa filamu ya La La Land walikuwa katikati ya hotuba yao ya kushinda taji hilo wakati makosa yalipogunduliwa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Emma Stone [nyuma} aonekana ameshangazwa na tangazo hilo

Filamu ya muziki ya La La Land ilishinda mataji sita ikiwemo mkurugenzi bora na muigizaji bora wa kike.

Moonlight pia ilishinda tuzo za muigizaji msaidizi bora.

Damien Chezelle mkurugenzi wa La La Land alikuwa mwandalizi mwenye umri mdogo wa filamu kushinda tuzo ya mkurugenzi bora akiwa na umri wa miaka 32.

Beatty na Dunaway walikuwa wametangaza La La Land kuwa mshindi wa filamu bora ,lakini mwandalizi Jordan Horowitz alitangaza kulikuwa na makosa.

Chanzo cha picha, KEVIN WINTER

Maelezo ya picha,

Beaty asijue la kufanya baada ya kugundua walifanya makosa

Alisema: Sio mzaha .Moonlight ndio filamu bora, huku akionyesha kamera kadi iliomtambua mshindi.

Waandalizi wawili wa filamu ya La La Land walikuwa wametoa hotuba zao kabla ya makosa hayo kugunduliwa.

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Maelezo ya picha,

Muigizaji wa Moonlight's Barry Jenkins na mwenzake wa La La Land Jordan Horowitz wakumbatiana baada ya makosa kurekebishwa

Mwandalizi Jimmy Kimmel alifanya mzaha kwamba alijua atafanya makosa akiifananisha hafla hiyo na kuongezea: Mimi mwenyewe namlaumu Steve Harvey kwa makosa haya akifananisha makosa ya Harvey wakati alipotangaza malkia wa urembo duniani 2015.