Aliyeolewa Uingereza kwa miaka 27 arudishwa kwao

Irene Clennel alikuwa akizuiliwa katika kituo kimoja cha Uskochi lakini ameambia BBC kwamba amerudishwa kwa bila kupewa onyo.
Maelezo ya picha,

Irene Clennel alikuwa akizuiliwa katika kituo kimoja cha Uskochi lakini ameambia BBC kwamba amerudishwa kwa bila kupewa onyo.

Mwanamke mmoja aliyeolewa na raia Muingereza kwa takriban miaka 27 amerudishwa kwao Singapore.

Irene Clennel alikuwa akizuiliwa katika kituo kimoja cha Uskochi lakini ameambia BBC kwamba amerudishwa kwa bila kupewa onyo.

Amekuwa akiishi karibu na Durham na mumewe na ana watoto wawili Waingereza mbali na mjukuu nchini humo.

Muda aliochukua kuwaangalia wazazi hao unadaiwa kufutilia mbali haki yake ya kuishi nchini humo.

Wizara ya maswala ya ndani haizungumzii kuhusu kesi za watu binafsi

Bi Clennel ambaye amekuwa akiishi Chester-le- Street alipewa likizo ya mara moja kusalia nchini Uingereza baada ya ndoa yake.

Anasema kuwa amefanya majaribio mengi akiwa nchini Singapore na Uingereza akitoa ombi la kuishi na mumewe.

Maelezo ya picha,

Alikuwa akizuiliwa katika kituo cha Dungavel

Bi Clennel anasema kuwa afya ya mumewe imezorota na kwamba yeye ndio mwangalizi wake.

Msemaji wa wizara ya maswala ya ndani nchini Uingereza amesema kuwa: Maombi yote ya kusalia Uingereza yanaangaziwa kibinafsi pamoja na sheria za uhamiaji. Tunatumai kwamba wale wasio na haki ya kuishi wataondoka.

Shirika la hisani la sauti ya wahamiaji linasema kuwa limeanzisha kampeni ya kumrudisha nchini Uingereza.

Mkurugenzi Nazek Ramadan amesema kuwa kisa chake ni mfano mwengine ambapo sera zinagawanya familia na kuharibu maisha.