Kwa picha: Tuzo za Oscars 2017

Baada ya nyota kuwasili katika Ukumbi wa Dolby mjini Los Angeles Tuzo hizo zilianza.
Maelezo ya picha,

Baada ya nyota kuwasili katika Ukumbi wa Dolby mjini Los Angeles Tuzo hizo zilianza.

Maelezo ya picha,

Justin Timberlake alianza hafla hiyo kwa kuwatumbuiza waliohudhuria kwa wimbo wake wa ulioteuliwa katika tuzo hizo Can't Stop The Feeling.

Maelezo ya picha,

Mwandalizi wa tuzo hizo Jimmy Kimmel alifanya mzaha aliposema kuwa tuzo hizo zinatazamwa na mataifa yanayochukia Marekani

Maelezo ya picha,

Mahershala Ali wa filamu ya Moonlight alishinda tuzo ya muigizaji msaidizi bora

Maelezo ya picha,

Mwanahesabati wa Nasa Katherine Johnson (wa pili kushoto anaonekana katika ukumbi na waigizaji Janelle Monae, Taraji P. Henson na Octavia Spencer

Maelezo ya picha,

Alessandro Bertolazzi, Giorgio Gregorini na Christopher Nelson walikubali tuzo za oscars kwa tuzo ya upambaji kwa filamu ya Suicide Squad.

Maelezo ya picha,

Colleen Atwood alishinda tuzo yake ya nne ya Oscar kwa filamu Fantastic Beasts and Where to Find Them, baada ya kushinda 2011 kwa filamu ya Alice in Wonderland, na 2006 kwa Memoirs of a Geisha huku 2003 akishinda filamu ya Chicago.

Maelezo ya picha,

Muigizaji Meryl Streep

Maelezo ya picha,

Na wakati waliohudhuria walipotaka kula, peremende zilianguka kutoka kwa paa la ukumbi huo

Maelezo ya picha,

Mzalishaji Caroline Waterlow na mkurugenzi Ezra Edelman wa OJ: Made in America wakichukua tuzo zao kwa makala bora

Maelezo ya picha,

Mchanganyaji wa sauti Kevin O'Connell akikubali tuzo aliyoshinda kwa Hacksaw Ridge

Maelezo ya picha,

Viola Davis alishinda tuzo ya muigizaji msaidizi kwa kucheza nafasi ya Rose kwa mchezo wa kuigiza Fences.

Maelezo ya picha,

Muigizaji Denzel washington akiwafungisha ndoa watalii wawili katika ukumbi huo wa Oscar

Maelezo ya picha,

Kimmel akimbeba muigizaji Sunny Pawar, kutoka Lion, wakati muziki kutoka kwa king ulipochezwa na kumfurahisha nyota mwenza Dev Patel.

Maelezo ya picha,

Muigizaji Hailee Steinfeld, wakurugenzi mwenza Byron Howard na Rich Moore pamoja na mzalishaji Clark Spencer,

Maelezo ya picha,

Seth Rogen (left) na Michael J. Fox wanatoka katika gari lao

Maelezo ya picha,

Mwandalizi wa Uingereza Joanna Natasegara na Mkurugenzi wa Uingereza r Orlando von Einsiedel wakisimama mbee ya ukumbi baada ya kushinda makala bora ya The White Helmets

Maelezo ya picha,

Waigizaji Ryan Gosling na Emma Stone

Maelezo ya picha,

Msanii John Legend akiwatumbuiza waliohudhuria katika tuzo za Oscars

Maelezo ya picha,

Muigizaji Salma Salma Hayek na mwandalizi Joanna Natasegara

Maelezo ya picha,

Amy Adams akimpatia tuzo ya Best Adapted Screenplay kwa Tarell Alvin McCraney na Barry Jenkins

Maelezo ya picha,

Casey Affleck ashtuka baadya kupewa tuzo muigizaji bora wa kiume

Maelezo ya picha,

La La Land ilishinda tuzo nyengine , mara hii ikiwa ni Emma Stone kwa kuwa muigizaji bora wa kike.

Maelezo ya picha,

Tuzo ya filamu bora ilikabidhiwa La La Land lakini bahasha iliopewa Warren Beaty aliyekuwa akitoa tuzo hiyo ilikuwa na makosa

Maelezo ya picha,

Kulikuwa na kelele kwa muda pale Jordan Horowitz wa La La Land aliposema kuwa tuzo hiyo ingepewa Moonlight

Maelezo ya picha,

Hali ya kawaida ilirejea baada ya waigizaji wa filamu ya Moonlight kufika mbele ya jukwaa ili kukubali tuzo ya filamu bora

Maelezo ya picha,

Picha ya mwisho inayomuonesha muigizaji musaidi bora Mahershala Ali, Muigizaji bora wa kike Emma Stone, MUigizaji msaidizi bora wa kike Viola Davis na muigizaji bora wa kiume Casey Affleck wakishika tuzo walizoshinda

All photographs subject to copyright.