Waandamanaji wapanda mgomba katikati ya barabara Nairobi

Haki miliki ya picha RamogiFM/TWITTER
Image caption Watoa huduma za usafiri wapanda mgomba wa ndizi barabarani Nairobi

Wahudumu wa magari ya usafiri nchi Kenya, yanayofahamika kama matatu wamefanya maandamano kulalamikia hali mbaya ya barabara kwenye mitaa ya mji mkuu Nairobi.

Kituo kimoja cha redio kimetuma picha ya waandamanaji wakipanda mgomba wa ndizi barabarani kwenye mtaa wa Kayole, kama njia ya kusema kuwa barabara iyo inaweza kuwa bora kwa kilimo kuliko iwe barabara ya magari.

Haki miliki ya picha RamogiFM/TWITTER
Image caption Watoa huduma za usafiri wapanda mgomba wa ndizi barabarani Nairobi