Zaidi ya Watanzania 5000 watoroka Msumbiji
Huwezi kusikiliza tena

Zaidi ya Watanzania 5000 watoroka Msumbiji

Idadi ya Watanzania waliokimbia Msumbiji imevuka 5000 kufikia ijumaa ya wiki iliyopita, kwa mujibu wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Watanzania hawa pamoja na raia wa nchi nyingine ikiwemo Somalia na Senegal walikuwa wakiishi na kufanya kazi katika eneo lenye madini ya rubi liitwalo Montepweshi, Kaskazini mwa Msumbiji.

Lakini wiki mbili zilizopita serikali ya eneo hilo ilitoa siku tano kwa raia wote wakigeni waishio hapo kuondoka mara moja.

Hata hivyo akiongea na BBC, mkurugenzi wa idara ya misitu na wanyapori kwenye mkoa wa Cabo Delgado nchini Musumbiji Abdul Chuguro, ametaja madai hayo kuwa yasiyo ya ukweli, lakini amethibitisha kuwa Watanzania na watu kutoka mataifa mengine wakiwemo raia wa Musumbiji walilazimiswa kuachana na uchimbaji madini ulio haramu wa rubi kwenye wilaya ya Montepuez.

Alisema kuwa kile kilichotwaliwa kutoka kwa raia wa Tanzania na magari 22 yaliyokosa usajili au yaliyokuwa na usajili bandia.

Katika upande wa madai ya ubakaji alisema kuwa kesi moja iliripotiwa lakini wakati ilipofanyiwa uchunguzi wa kiafya madai hayo yaligunduliwa kuwa ya uongo.

Sammy Awami alikwenda mpakani mwa Tanzania na Msumbuji na kutuandalia taarifa ifuatayo