Ndege za Israel zashambulia wapiganaji wa Hamas Gaza

Ndege za kivita za Israel zashambulia maficho ya wapiganaji wa Hamas Gaza

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Ndege za kivita za Israel zashambulia maficho ya wapiganaji wa Hamas Gaza

Ndege za kivita za Israeli, zimelenga maeneo kadhaa yanayoaminika kutumika na wapiganaji katika maeneo ya ukanda wa Gaza.

Ripoti ya vyombo vya habari nchini humo, zinasema kuwa mengi ya maeneo hayo yaliyopigwa na mabomu, yanamilikiwa na vuguvugu la wapiganaji wa Hamas.

Eneo moja linalotumika na wapiganaji wanaojiita Islamic Jihad, pia limepigwa bomu.

Yamkini watu watatu wamejeruhiwa katika mashambulio hayo.

Jeshi la Israeli limesema kuwa, mashambulio hayo ya hivi punde, ni kujibu kisasi cha kurushwa kwa maroketi kutoka Gaza hadi maeneo ya ndani kusini mwa Israeli.