Mkenya afariki katika mashindano ya kilimanjaro

Mkenya afariki katika mashindano ya kilimanjaro
Maelezo ya picha,

Mkenya afariki katika mashindano ya kilimanjaro

Waziri wa habari , utamaduni, sanaa na michezo nchini Tanzania Nape Moses Nnauye ametoa salamu za pole kwa Rais wa shirikisho la riadha nchini humo, kufuatia kifo cha mshiriki kutoka nchini Kenya, ambaye alifariki katika mashindano ya kilimanjaro Marathon, yaiyofanyika tarehe 26 mwezi huu mkoani Kilimanjaro.

Bwana Charles Rioba, mwenye umri wa miaka 36, alishiriki mbio za kilomita 21 kwa hiyari, zilizohusisha wananchi wote kwa ujumla wakiwemo viongozi wastaafu zijulikanazo kama "run for fun".

Akiwa katika mbio hizo Bwana Rioba alianguka na kupatiwa huduma ya kwanza na kupelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Kilimanjaro na baadaye kufariki dunia.