Azania Group, kuiwakilisha Tanzania mashindano ya kikanda

Tanzania Haki miliki ya picha Google
Image caption Timu Azania Group

Timu ya Azania Group, ndiyo itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya Afrika Mashariki, ya Benki ya "Standard Chartered-Road to Anfield" yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi, Machi 4.

Azania walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy mabao ya 6-5 kwa penati dhidi ya katika mchezo wa kukata na shoka uliofanyika mwishoni mwa wiki na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania.

Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda.

Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola wakati kidedea wa kombe hilo nchini Kenya ni Radio ya Capital FM.