Space X kuwasafirisha watalii 2 mwezini 2018

Watalii wawili kwenda mwezini 2018

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Watalii wawili kwenda mwezini 2018

Kampuni ya kibinafsi ya kurusha roketi imetangaza kwamba watalii wawili wamelipa kupelekwa mwezini.

Safari hiyo itafanyika 2018 kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SpaceX Elon Musk, alieongezea kwamba watalii hao tayari wamelipa kiasi fulani cha fedha.

''Hatua hiyo inatoa fursa kwa binaadamu kurudi katika anga za juu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45'',alisema.

Wawili hao ambao majina yao hayakutajwa wataelekea mwezini wakiwa katika meli hiyo ya angani ambayo itafanyiwa jaribio lake la kwanza la kurusha rekoti isiokuwa na rubani.

Bwana Musk alisema kuwa ushirikiano wa shirika la sayansi na teknolojia ya angani nchini Marekani Nasa umefanya ufanisi wa safari hiyo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Roketi itakayotumika kuwasafirisha watalii hao

Amesema kuwa abiria hao wawili watasafirishwa kwa kasi zaidi ya watu wengine wowote kuwahi kusafirishwa katika sayari.

Bwana Musk hatahivyo amekataa kuwataja abiria hao wawili ,akisema kwamba ni watu wanaojuana na kwamba hawatoki Hollywood.

Kama wanaanga wa Apollo, wawili hao watasaifiri angani wakibeba matumaini na ndoto za binaadamu wote wanaopenda kusafiri.

Tunataraji kuwafanyia ukaguzi wa kiafya kabla ya kuanza kuwafunza baadaye mwaka huu.