UNICEF: Watoto wahamiaji wanyanyaswa Libya

UNICEF inasema kuwa watoto hunyanyaswa Libya katika harakati za kuelekea Itali

Chanzo cha picha, UNICEF

Maelezo ya picha,

UNICEF inasema kuwa watoto hunyanyaswa Libya katika harakati za kuelekea Itali

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba idadi kubwa ya watoto wanaendelea kuhatarisha maisha yao, kwa kuvuka bahari ya mediterania kutoka Libya hadi Italia.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF, linasema watoto 26,000, wengi wao wakiwa bila walezi, walivuka bahari ya mediterania mwaka jana.

Idadi hiyo ni mara dufu ikilinganishwa na mwaka 2015.

Chanzo cha picha, UNICEF

Maelezo ya picha,

Watoto hukabiliwa na tisho la kufnywa makahaba na magenge ya uhalifu

Katika ripoti mpya, UNICEF, inasema watoto hao wanadhulumiwa na kunyanyaswa kimapenzi na walanguzi wa binadamu, japo huwa hawatoi ripoti kwa polisi kwa hofu ya kutiwa mbaroni na kurejeshwa Libya.