Aomba msamaha kwa kuwaita wahamiaji ''funza''

Uhamiaji katika bahari ya pacific

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uhamiaji katika bahari ya pacific

Mwansiasa mmoja wa Australia ameomba msamaha baada ya kuwaita wahamiaji ''funza''.

David Fawcet ,seneta wa serikali alitoa matamshi hayo wakati wa kikao cha bunge siku ya Jumatatu.

Katika mjadala kuhusu kuwasili kwa maboti ya wahamaiji ,bw Fawcet alikishtumu chama cha upinzani cha leba kwa kuzua swala la ''funza''.

Baadaye aliomba msamaha kwa kutumia neno hilo akidai kwamba halikuwalenga wahamiaji.

''Nimezungumza kwa simu na bw Phil Glandenning ,rais wa baraza la wakimbizi nchini Australia .Ameniambia kwamba maneno niliotamka mapema yamechukuliwa vibaya na kusababisha uchungu mwingi miongoni mwa jamii ambayo baraza lake linawakilisha, na nikaamua kuomba msamaha''.

Australia imekuwa na sera yenye utata ya kuwazuilia wakimbizi wanaowasili kwa maboti katika vituo vya kuwazuilia wahamiaji karibu na taifa la pacific la Nauru na Papua New Guniea.