Mtoto akwama mgodini kwa siku 3 Afrika Kusini

Mtoto aliyekwama mgodini siku 3 Afrika Kusini kuokolewa Haki miliki ya picha Pelane Phakgadi/EWN
Image caption Mtoto aliyekwama mgodini siku 3 Afrika Kusini kuokolewa

Jitihada za uokoaji zinatarajiwa kuendelea kumuokoa mtoto wa umri wa miaka mitano ambaye amekwama kwa karibu siku tatu kwenye mgodi moja usiotumiwa eneo la Boksburg, ambao ni mji ulio nje ya jiji la Johannesburg.

Inaripotiwa kuwa mtoto huyo alianguka ndani ya shimo hilo siku ya Jumamosi.

Kulingana na shirika la EyeWitness News, shughuli hiyo ya kumtafuta ilisitishwa siku ya Jumatatu usiku, baada wa waokoaji kukumbwa na matatizo ya kupumua wakiwa chini ya ardhi.

Baadhi ya wenyeji wanasema kuwa wametoa wito wa kutaka kufungwa kwa shimo hilo kwa miaka mingi.

Watu wengi wanatarajiwa kukusanyika tena kutazama shughuli ya kumuokoa mtoto huyo.