Aliyejiongezea mshahara mkubwa Afrika Kusini afutwa kazi

Aliyejiongezea mshahara mkubwa Afrika Kusini afutwa kazi

Chanzo cha picha, Thinkstock

Maelezo ya picha,

Aliyejiongezea mshahara mkubwa Afrika Kusini afutwa kazi

Afisa mmoja wa serikali nchini Afrika Kusini ambaye alijiongezea mshahara wa asilimia 350 amefutwa kazi.

Collins Letsoalo alipewa wadhifa huo ili apate kukabiliana la ulaji ruswa na pia aliboreshe shirika la reli la Afrika Kusini linalokumbwa na matatizo.

Lakini muda mfupi baada ya kuchukua wadhifa wake mwaka uliopita, alijiongezea mshahara kwa asilimia 350 na kuufikisha hadi dola 450,000 kwa mwaka.

Wakati gazeti lilichapisha taarifa kuhusu kile kilichotajwa kuwa nyongeza isiyo halali, bwana Letsoala alisisitiza kuwa hakufanya lolote baya.

Lakini bodi ya shirika hilo la reli sasa imeamua kumfuta kazi.

Huku uchumi wa Afrika Kusini ukiwa umekwama na serikali ikiwa inakopa zaidi kulipa wafanyakazi wake wengi, watu wanastahili kujifunza kutokana kuanguka kwa bwana Letsoalo.