Uchumi wa Nigeria ulishuka zaidi mwaka uliopita

Uchumi wa Nigeria ulishuka zaidi mwaka uliopita

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Uchumi wa Nigeria ulishuka zaidi mwaka uliopita

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa uchumi wa Nigeria ulishuka kwa asilimia 1.5 mwaka jana wa 2016, huku taifa hilo likikabiliwa na hali mbaya ya mdororo wa uchumi.

Mwaka jana, taifa hilo kubwa kiuchumi barani Afrika, lilikumbwa na hali ngumu zaidi ya maisha kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita, kufuatia kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

Ripoti kutoka kwa idara inayoratibu takwimu nchini Nigeria, inasema kuwa kushuka huku kwa uchumi, kunaashiria mwaka mgumu kwa Nigeria, pamoja na kushuka kwa mahitaji, matatizo katika sekta ya nishati na sarafu dhaifu.

Wakosoaji wa serikali wanasema kuwa sera mpya za serikali, zimesababisha hali kuwa hata mbaya zaidi.