Trump amlaumu Obama kwa maandamano

Trump amlaumu Obama kwa maandamano
Image caption Trump amlaumu Obama kwa maandamano

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini kuwa Barack Obama ndiye anahusika na maandamano dhidi ya uongozi wa Republican.

"Nafikiri Rais Obama anahusika kwa sababu ni watu wake wanaohusika kwenye maandamanohayo," Trump alikiambia kituo cha Fox News.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Trump alikuwa akiongea na kituo cha Fox News

Trump hakutoa ushahidi wowote kwa madai yake na Obama bado hajajibu lolote.

Trump pia alizungumzia bajeti na masuala mengine.

Alipoulizwa kuhusu maandamano yanayohusu amri ya kusaka. alisema kuwa ni wafuasi wa Obama waliohusika.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump anasema ataongeza bajeti ya jeshi kwa asilimia 10