Watu asilimia 30 wanakabiliwa na njaa Uganda

Watu asilimia 30 wanakabiliwa na njaa Uganda

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Watu asilimia 30 wanakabiliwa na njaa Uganda

Serikali ya Uganda, inasema kuwa asilimia 30 ya idadi nzima ya raia nchini humo, wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula kwa sababu ya baa la njaa.

Hayo yametukia baada ya muda mrefu wa ukame kukithiri katika maeneo mengi nchini humo, mbali na mataifa jirani ya Afrika mashariki.

Watu wengi wana matatizo makubwa ya kupata chakula kutokana na mavuno mabaya msimu uliopita, ugonjwa uliotatiza mimea na viwango vikubwa vya bei ya chakula.

Serikali imeahidi kuwasaidia watu walioathirika na ukame huo.