Mwalimu amsaidia mwanafunzi na figo yake

Madaktari wakitoa figo Haki miliki ya picha Spl
Image caption Madaktari wakitoa figo

Mwalimu wa chekechea nchini Marekani, ameelezea furaha aliyokuwa nayo kwa kuweza kumsaidia mwanafunzi wa miaka mitano kwa kumpa mtoto huyo moja ya figo zake.

Beth Battista ameiambia BBC kwamba hakusita kutoa figo yake baada ya kusikia jitihada za Lyla za kutafuta figo kwa muda mrefu.

Mwalimu huyo, ambae pia ni mama wa watoto wawili, amesema alisikia kuhusu hali ya Lyla baada ya mamake kuweka taarifa za mwanawe katika mtandao wa Facebook.

Mwaka mmoja uliopita, Lyla alipatikana na tatizo la figo ambapo alitakiwa kusafishwa damu kwa saa kumi na mbili kwa siku.