Wanawake wakabiliwa na ukatili dhidi yao Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake wanaopigwa na wanaume zao Tanzania

Moja ya changamoto wanayokumbana nayo wanawake walioko katika ndoa kwenye baadhi ya makabila nchini Tanzania, ni kipigo kutoka kwa waume zao, Lakini Wanawake wengi walioathiriwa na vitendo hivyo hawatoi taarifa kwa vyombo husika kutokana na utegemezi wa kiuchumi walio nao na utamaduni wa jamii zao.

Takwimu za hivi karibuni kutoka taasisi ya utafiti ya Repoa nchini Tanzania, imesema kuwa asilimia thelathini ya wanawake wanakabiliwa na vitendo vya ukatili dhidi yao.

Kuna imani pia miongoni mwa baadhi ya jamii kama vile Wakurya kwamba kumpiga mwanamke kunasaidia kuwaweka katika maadili mema na pia ni njia ya kuonyesha upendo.

Utamaduni wa aina hii unakwaza mapambano dhidi ya unyanyasaji huo.

Mwandishi wetu Munira Hussein alizungumza na baadhi ya wanawake waliopitia visa hivyo na kuandaa taarifa ifuatayo.