Facebook yafuta michoro ya utupu

Women Lovers, ulichorwa na Charles Blackman Haki miliki ya picha Mossgreen
Image caption Women Lovers, ulichorwa na Charles Blackman

Facebook imezuia duka moja la michoro nchini Australia kuchapisha michoro ya utupu.

Michoro hiyo ya Charles Blackman inayojulikana kama Women Lovers, inaonyesha wanawake wawili walio uchi ambao wako kitandani kando mwa paka.

Muuza michoro Mossgreen, alijaribu kuutangaza mchoro huo kupitia Facebook lakini mtandao huo ukakataa.

Mkurugenzi mkuu wa Mossgreen Paul Summer, anaitaja hatua hiyo ya Facebook kama ya kushangaza.

Facebook inasema kuwa uamuzi wake ndio wa mwisho lakini Mossgreen ameichapisha tena michoro hiyo.

Mwezi uiopita mwalimu mmoja nchini Ufaransa aliushtaki mtandao wa Facebook, kwa kufuta ukurasa wake baada ya kuchapisha picha ya utupu ya mwanamke iliyochorwa karne ya 19.

Bwana Summer anasema mchoro huo wa Women Lovers, ulitarajiwa kuuzwa kwa zaidi ya dola 34,000 wiki ijayo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Blackman na bintiye Christabel mwaka 2005