Mtoto aliyeanguka mgodini Afrika Kusini bado anatafutwa

Mtoto aliyetoweka Afrika Kusini bado atafutwa
Image caption Mtoto aliyetoweka Afrika Kusini bado atafutwa

Waokoaji nchini Afrika Kusini wanaendelea kumtafuta mtoto mvulana wa umri wa miaka mitano, ambaye alianguka ndani ya mgodi usiotumika eneo moja mashariki mwa mji wa Johannesburg.

Inaaminiwa kuwa Richard Thole alitoweka alipokuwa akicheza na marafiki zake siku ya Jumamosi.

Mamia ya watu wamekusanyika eneo hilo licha ya onyo kutolewa kuwa eneo lenyewe ni hatari.

Wenyeji wanawalaumu waokoaji kwa kutofanya hima kumpata mtoto huyo.

Wengine wamefunga barabara na kuchoma magurudumu wakiitaka serikali iwahamishe kuenda eneo lililo salama.