Afrika Kusini yawafukuza mamia ya raia wa kigeni

Wahamiaji wamekuwa wakishambuliwa Afrika Kusini

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wahamiaji wamekuwa wakishambuliwa Afrika Kusini

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Afrika Kusini imethibitisha ripoti kuwa raia kadha wa Nigeria wamefukuzwa kutoka nchini humo.

Vyombo vya habari nchini Nigeria vimekuwa vikiripoti kuwa raia 97 wa Nigeria wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu tofauti walifukuzwa kutoka Afrika Kusini siku ya Jumatatu.

Msemaji wa wizara hiyi Mayihlome Tshwete anasema kuwa mamia ya watu wasio na vibali walisafirishwa kutoka nchini humo, wengi wao kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Wahamiaji walijihami kujilinda Afrika Kusini

Wengine ni raia wa Pakistan, China, Bangladesh na Somalia.

Afrika Kusini imekumbwa na ghasia dhidi ya raia wa kigeni na visa vya kuporwa kwa maduka yanayomilikiwa na wahamiaji.

Afrika Kusini huwafukuza karibu watu 30,000 kila mwaka.