Dawa zinazotibu mifupa iliodhoofika zatiliwa shaka

licha ya dawa hiyo kuonekana kutibu ugonjwa huo, huenda ikasababisha nyufa zaidi katika mifupa
Image caption licha ya dawa hiyo kuonekana kutibu ugonjwa huo, huenda ikasababisha nyufa zaidi katika mifupa

Utafiti mpya unasema kuwa dawa zinazotumiwa kutibu mifupa iliodhoofika miongoni mwa wagonjwa wenye umri mkubwa huenda zinazidi kuidhoofisha mifupa yao.

Utafiti huo uliofanywa na wanasayansi katika taasisi ya chuo cha Imperial mjini London ,ilichunguza mifupa ilivyotengezwa kutoka kwa mgonjwa aliyetibiwa na dawa ya bisphosphonates baada ya kuvunjika mfupa wa kiuno.

Ulibaini kwamba licha ya dawa hiyo kuonekana kutibu ugonjwa huo, huenda ikasababisha nyufa katika mifupa ambayo inapunguza nguvu za mifupa hiyo kufanya kazi.

Wanasayansi wanasema kuwa utafiti zaidi unahitajika na kwamba wagonjwa hawafai kuwacha kutumia dawa wanazopewa na madaktari wao.

Ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa huwaathiri zaidi ya watu milioni 200 duniani.