Waziri mkuu wa Somalia aidhinishwa na bunge

Waziri mkuu wa Somalia aidhinishwa rasmi na bunge
Image caption Waziri mkuu wa Somalia aidhinishwa rasmi na bunge

Bunge la Somalia limeidhinisha uteuzi wa Hassan Ali Kheyra kuwa waziri mkuu.

Kheyra ambaye aliwahi kufanya kazi kama mshauri na mkurugeni mkuu wa kampuni ya mafuta anatarajiwa kuteua baraza lake la mawaziri.

Akihutubia bunge, alisema kuwa lengo lake kuu ni kukabiliana na ukame uliopo, kuimarisha usalama mbali na kukabiliana na ufisadi.

Hatahivyo kazi ya mkuu huyo wa serikali ya Somalia huenda ikapungua baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kwamba Somalia ipo katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa pamoja na tishio la usalama linalotolewa na kundi la wapiganaji wa al-Shabab.