Waasi wa FARC waweka silaha chini

Colombia
Image caption Ivan Marquez kutoka upande wa FARC na Humberto de la Calle wakipeana mkono wa amani

Waasi wa FARC nchini Colombia wameanza kukabidhi silaha zao kwa waangalizi wa umoja wa mataifa kama sehemu ya mkubaliano ya usitishwaji wa mgogoro uliosainiwa mwezi Novemba mwaka 2016.

Kamishna wa amani Sergio Jaramillo amesema kuwa serikali inatarajia kupokea maelfu ya silaha kutoka kwa waasi wa FARC ndani ya miezi mitatu ijayo.

Baada ya kukabidhi silaha hizo waasi wa FARC wataruhusiwa kuondoka katika maeneo waliyokusanyika ambapo wanaishi kama raia wengine.

Kundi la pili kwa ukubwa nchini Colombia ELN walianza mazungumzo ya amani na serikali ya nchi hiyo mwezi uliopita.