CIA kuchunguza iwapo Urusi ilingilia uchaguzi wa Marekani

Picha ya rais Vladmir Putin na Donald Trump .Wapinzani wa Trump wanamtuhumu kuhusu uhusiano wake na Putin Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Picha ya rais Vladmir Putin na Donald Trump .Wapinzani wa Trump wanamtuhumu kuhusu uhusiano wake na Putin

Mwenyekiti wa kamati ya ujasusi katika bunge la Congress ambaye ni mwanachama wa Republican, Devin Nunes amesema wanachunguza ikiwa kulikua na ushirikiano wa kina kati ya Urusi na baadhi ya raia wa Marekani.

Taarifa hii inamaanisha kwamba suala la mchango wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani linaendelea kutiliwa manaani.

Kamati ya ujasusi katika baraza la Congress imekua ikiichunguza Urusi kwa miaka mingi na wakati huu inalenga kubaini ikiwa kulikua na shughuli zozote za Urusi katika uchaguzi wa Marekani .

Tayari Idara ya FBI inachunguza muingilio wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Shirika la Ujasusi CIA na imekiri kwamba utawala wa Vladimr Putin ulinuia kusaidia Donald Trump kumharibia sifa mpinzani wake Hillary Clinton.

Donald Trump na timu yake wamekanusha kuwa baadhi ya watu kwenye timu ya Trump waliwasiliana na maafisa wa Urusi kabla ya Uchaguzi Mkuu.