Mkufunzi wa Barcelona kubwaga manyanga

Mkufunzi wa Barcelona Louis Enrique amesema kuwa atajiuzulu mwishoni mwa msimu huu ili kupumzika Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkufunzi wa Barcelona Louis Enrique amesema kuwa atajiuzulu mwishoni mwa msimu huu ili kupumzika

Mkufunzi wa klabu ya Barcelona Luis Enrique ametangaza kwamba atabwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu.

Enrique atakuwa amehudumu kama meneja wa klabu hiyo kwa misimu mitatu .

Aliishindia klabu hiyo kombe la vilabu bingwa na mataji mengine mawili alipojiunga na Barcelona na kuwasaidia kushinda makombe 2 mwaka uliopita.

Lakini licha ya klabu hiyo kuongoa katika jedwali la ligi Barcelona iko katika hatari ya kubanduliwa katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu huu baada ya kufungwa 4-0 na Prais St-Germain.

Enrique amesema kuwa sababu kuu ya yeye kutaka kujiuzulu ni kwamba anahitaji kupumzika.