UN: Watu 40 walifariki katika maandamano dhidi ya Kabila DRC
Huwezi kusikiliza tena

UN: Watu 40 walifariki katika maandamano dhidi ya Kabila DR Congo

Takriban watu 40 waliuawa na zaidi ya 140 kujeruhiwa , kulingana na ripoti ya pamoja ya Umoja wa mataifa na tume ya haki za kibinaadamu nchini DR Congo.

Watu hao wanadaiwa kuuawa mnamo tarehe 19 Disemba mwaka jana na vikosi vya usalama wakati walipojaribu kufanya maandamano ya kuishinikiza serikali ya rais Joseph Kabila kuachia madaraka.

Tarehe hiyo ilikuwa mwisho wa muhula wake kulingana na katiba.

Mbelechi Msoshi anaarifu zaidi kutoka kinshasa.