Uoshaji vyombo wamfanya kumiliki mgahawa Denmark

Ali Sonko Haki miliki ya picha EPA
Image caption Muoshaji vyombo Ali Sonko

Muoshaji wa vyombo katika mgahawa uliozawadiwa mara nne kuwa mgahawa bora ulimwenguni amepandishwa daraja na kuwa mmiliki mwenza wa mgahawa huo.

Ali Sonko , 62, kwa hivi sasa ni mshirika wa mkahawa wa Noma ulioko Copenhagen ambapo amekuwa akihudumu tangu ulipofunguliwa.

Bw Sonko kutoka Gambia aliwasilishwa miongoni mwa washirika wengine watatu wapya , pamoja na mameneja wawili.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mpishi Rene Redzepi

''Ali ni moyo wa Noma'' mpishi Rene Redzepi aliwaelezea marafiki waliokongamana kusherekea mgahawa huo , Kulingana na gazeti la Ujerumani la Berlingske.

''Sidhani kama watu hushukuru kuwa na mtu kama Ali , yeye hutabasamu licha ya hali ya watoto wake 12 wanavyoendelea.

''Hata mimi babangu alikuwa akiitwa Ali , pia yeye alifanya kazi ya uoshaji vyombo alipokuwa mnjini Denmark. Redzepi alisema

Bw Sonko ameishi Denmark kwa miaka 34 , alipata umaarufu mwaka 2010, pale aliposhindwa kuelekea na wenzake mjini London kupokea tuzo yao ya kwanza ya kuwa mgahawa bora kote ulimwenguni.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ali Sonko na Redzepi

Lakini wenzake kutoka Noma , hawakumsahau , na badala yake walivalia mashati yaliokuwa na uso wa muoshaji huyo wa vyombo , na miaka miwili baadaye , shida ya visa yake ikatatuliwa na Sonko akapata nafasi ya kutoa hotuba ya kukubali ushindi wa kuwa mgahawa bora ulimwenguni kwa mara ya pili.

''Siwezi kueleza furaha niliyo nayo ya kufanya kazi hapa,'' Sonko alisema.

''Hawa ni watu wazuri kufanya nao kazi , mimi ni rafiki wa kila mmoja .watu hawa wamenipatia heshima kubwa , haijalishi ninachosema au kuuliza , huniunga mkono , na kwa hayo nasema hii ni kazi nzuri sijawahi fanya maishani mwangu.''