Oprah Winfrey kuwania urais Marekani?

Bi Oprah Winfrey Haki miliki ya picha AP
Image caption Bi Oprah Winfrey

Oprah Winfrey huenda akawania urais kufuatia hatua ya rais Donald Trump kushinda urais.

Aliambia runinga ya Bloomberg kwamba kuchaguliwa kwa Trump licha ya yeye kukosa uzoefu wowote wa kisiasa kumemfanya kufikiria kuhusu uwezo wake wa afisi hiyo kuu.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 63 ambaye amekuwa akishiriki katika kipindi cha mazungumzo na ambaye alimuunga mkono Hillary Clinton awali alikuwa akifutilia mbali maswali ya yeye kuingia siasa.

Lakini sasa ametoa ishara ya kutaka kua mgombea wa wadhfa huo.

''Sikufikria swala hilo hata kidogo'', aliambia mfadhili David Rubenstein katika kipindi chake katika runinga ya Bloomberg alipoulizwa iwapo atakubali kuwania wadhfa huo.''Nilifikiria,Oh.. Oh''?

Akimfananisha na Trump ,bw Rubenstein alisema kuwa sio kwamba mtu anahitaji uzoefu wa kuwa serikalini kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani.

''Hivyo ndivyo nilivyofikiri, aliongezea nilidhani sina uzoefu, sina ufahamu mwingi, aliongezea, nilifikiri ..Oh sina uzoefu mwingi na sasa nafikiria Oh''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bi Winfrey Oprah wakati wa kampeni za rais Barrack Obama nchini Marekani

Winfrey alimuunga mkono rais Barrack Obama mwaka 2008 ambapo wengi walisema kuwa hatua hiyo ilimpiga jeki katika uchaguzi wa kutaka kuteuliwa dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu bi Clinton.

Pia alimuidhinisha bi Clinton kuwania urais mwaka 2016.

Kuna wakati mmoja Bw Trump alipendekeza Clinton kuwa makamu wake 1999, na mara nyengine mwaka uliopita alisema kwamba angependa bi Oprah kuwa katika tiketi yake ya kuwania urais.

Lakini Winfrey kwa mara nyingi amekuwa akipinga kuingia katika siasa kama mgombea .

Pia kumekuwa na uvumi kwamba mmiliki wa facebook Mark Zickerbag ,msanii wa mtindo wa Rap Kanye West na makurugenzi wa Disney Bob Iger huenda wakawania wadhfa huo mkuu.