Mahasibu wa Oscar waliokanganya watu kutoshirikishwa tena

Bw Cullinan mmoja ya mahasibu wa kampuni ya PricewaterHouseCoopers waliokanganya watu katika tuzo za Oscars Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bw Cullinan mmoja ya mahasibu wa kampuni ya PricewaterHouseCoopers waliokanganya watu katika tuzo za Oscars

Mahasibu wawili waliohusika na ukanganyaji wa bahasha za ushindi katika tuzo za Oscar hawataruhusiwa tena kushiriki katika tuzo hizo, rais wa Oscars ametangaza.

Cheryl Boone Issac alisema kuwa uhusiano wao na kampuni ya uhasibu ya PriceWaterhouseCoopers PWC pia unaangaziwa upya.

Brian Cullinan na Martha Ruiz walihusika na tatizo lililokuwa siku ya jumapili.

La La Land ilitajwa kimakosa kuwa mshindi wa tuzo la filamu yenye picha bora badala ya mshindi wa tuzo hiyo Moonlight.

Kundi la wawakilishi wa filamu ya La La Land lilikuwa katikati ya hotuba zao kabla ya mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa.

Hatua hiyo imetajwa kuwa makosa makubwa kwa kipindi cha miaka 89 ya historia ya tuzo hizo .

Bw Cullinan alitoa kwa makosa bahasha kwa watangazaji wawili waliokuwepo.

Aliwapatia Warren Beaty na Faye Dunaway bahasha ya muigizaji bora badala ya bahasha iliokuwa na jina la filamu bora.

Kampuni ya PriceWaterhouseCoopers, ambayo huisabu kura na kuweka majina ya washindi katika bahasha hizo imeomba msamaha kwa mkanganyo huo.

Bwana Culinnan alichapisha ujumbe wa mshindi wa taji la muigizaji bora kwa wanawake Emma Stone kabla ya kutoa bahasha iliowakanganya waliokuwa katika hafla hiyo.