Matumaini ya kumpata mtoto aliyetoweka Afrika Kusini yadidimia

Richard Thole alianguka kwenye mgodi karibu wiki moja iliyopita
Image caption Richard Thole alianguka kwenye mgodi karibu wiki moja iliyopita

Matumaini yanazidi kudidimia Afrika Kusini kwa familia ya mtoto wa umri wa miaka mitano, ambaye alianguka ndani ya mgodi usiotumika, baada ya majaribio ya kumuokoa kushindikana.

Richard Thole, alikuwa akicheza karibu na nyumba ya familia ili karibu karibu na mji wa Johannesburg, wakati ardhi ilipoporomoka siku ya Jumamosi.

"Inaumiza, nafikiri mtoto wangu amekufa, Ninataka tu arudi akiwa hai au amekufa," mama yake mtoto huyo alisema.

Mji wa Johannesburg una migodi isiyotumiwa kufuatia uchumbaji wa dhahabu wa karne ya 19 ambao ulisababisha kupatikana kwa mji huo.

Haki miliki ya picha Maile Matsimela/BoksburgAdvertiser
Image caption Nombeko Thole and Meshack Mohlala wanapoteza matumaini ya mtoto wao kuokolewa akiwa hai

Sasa jeshi limeombwa kusaidia kumtafuta mtoto huyo.

Jitihada za uokoaji zimekuwa za mwendo wa chini kutokana na ardhi kutokuwa imara na maji yaliyo na kemikali ndani ya migodi.

Mzwandile Masina, ambaye ni meya wa wilaya ya Ekurhuleni, anasema kuwa kuna asilimia 11 ya hewa ndani ya mgodi, na itakuwa vigumu kwa mtoto huyo kuwa hai hadi sasa.

Wenyeji wa eneo hilo linalojulikana kama Jerusalem sasa wanataka serikali kuwahamisha wakisema kuwa wanahofia maisha yao.

Image caption Watu wengi wamekuwa wakitazama jitihada za uokoaji