Bashir amteua makamu wake kuwa waziri mkuu

Bakri Hassan Saleh ameteuliwa waziri mkuu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bakri Hassan Saleh ameteuliwa waziri mkuu

Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, amemteuwa makamu wake wa rais Bakri Hassan Saleh kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.

Kuna madai kwamba Bwana Bashir anamuandaa awe mrithi wake.

Bwana Saleh ni mmoja wa mshirika wa karibu zaidi wa Bashir, na alihusika katika mapinduzi ya mwaka 1989 yaliyomleta mamlakani Omar Al Bashir.

Huku wakiwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa upinzani na jamii ya kimataifa, Bwana Mr Bashir amebuni cheo cha waziri mkuu, ambacho aliifutilia mbali mara tu baada ya kuingia uongozini kwa njia ya mapinduzi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Omar al-Bashir