Kwa Picha : Kuhifadhi turathi za kisiwani Zanzibar

Majumba yaliyoko pwani mwa Tanzania, kisiwa cha Zanzibar yanaangazia usanifu wa ujenzi wa waswahili.

Baada ya miaka mingi ya kutelekezwa , majumba mengi yameporomoka.

Kwa sasa, kundi dogo la mafundi wanajaribu kutumia mbinu na maarifa ya jadi kuhifadhi majumba hayo

Mwanamume anapeleka baiskeli mjini Zanzibar Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville
Mlango wa kitamaduni ya Zanzibar Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville
Mji mkuu wa Zanzibarl, Stone Town Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville

Stone Town, eneo la kihistoria la mji mkuu wa Zanzibar, lilitajwa na shirika la umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni ,UNESCO kuwa la kihistoria mwaka 2000.

Hata hivyo ni eneo lililoatharika kutokana na ongezeko la watu , msongamano wa magari na hali ya hewa kwenye kisiwa hicho.

Palace ya Mtoni Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville

Utumiaji ya saruji, kwa ukarabati, badala ya mchanga wa kale uliochanganywa na chokaa, umeongezea kupungua kwa nyumba nyingi kama ya the palace of Mtoni

Students working on a damaged doorway Wanafunzi wakiukarabati mlango Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville
Wanaurekebisha mlango Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville
Mlango wa kale wa Zanzibar Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville

Wanafunzi wa Zanzibar, waliopata mafunzo ya useremala na uashi walianzisha mradi wa kujenga majumba hayo ya urithi, kwa lengo la kuhifadhi majengo

Omar Yussuf Abdalla , mwenye umri wa miaka 38 , amesema kuwa mafunzo haya yatanilipa mshahara na kusaidi maisha yangu.

''Itawanisaidia mimi kuwafundisha wenzangu mbinu za kuhifadhi tamaduni zetu na mlango wa Stone Town.''

Nyumba ya kale , Stone Town Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville
Mhadhiri wa Ufundi ,Vuaa Khamis Mtumwa, Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville
Ndani ya nyumba iliyobomoka Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville
Jumba la Stone Town Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d'Unienville

Picha na Aurelie Marrier d'Unienville

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii