Marekani yawashambulia Al- Qaeda

Yemen
Image caption Kizuizi cha njiani

Marekani imefanya mashambulizi ya anga zaidi ya ishirini katika maeneo yanayodhaniwa kuwa yako chini ya himaya ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda huko Yemen. Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini Marekani amesema kuwa mashambulizi hayo yaliwalenga wapiganaji wa Al-Qaeda, vifaa vyao na na miundominu katika sehemu tatu za nchi hiyo.

Mwezi uliopita Rais wa Marekani Donald Trump alitoa maamuzi ya kwanza ya kufanyika kwa shambulio huko Yemen chini ya Utawala wake.

Mwanajeshi mmoja wa Marekani aliuawa katika operesheni hiyo. Taarifa mbalimbali zinaonesha kuwa idadi kubwa ya watoto na wanawake wamekufa katika operesheni hizo.